Powered by Blogger.

Kipigo cha PSG dhidi ya Man United chamchanganya Star wa Brazil Neymar


Man United imefanikiwa kupindua matokeo ugenini kwa kuichapa PSG mabao 3-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 3-3 Man United ikinufaika kwa faida ya kuwa na magoli mengi ya ugenini.


Kwenye mchezo wa Jumatano hii, mabao ya Man United yamefungwa Lukaku dakika ya 2 na 30 huku Rashford akimalizia kwa mkwaju wa penati dakika ya 90, wakati bao pekee la wenyeji limefungwa na Bernat dakika ya 12.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nyumbani kwa Man United, PSG ilishinda mabao 2-0.
Baada ya mchezo huo kumalizika kwa PSG kutupwa nje ya UEFA , Neymar ambaye alikuwa nje kwa majeruhi alitoa lawama kuhusu penati ya dakika za mwisho ambayo walipema Man United na kufanikiwa kupata goli la ushindi.
“That is a disgrace!” aliandika Neymar kupitia instastory ya instagram yake.
Aliongeza, “And UEFA still pick four guys who know nothing about football to review the VAR decision in slow motion… that handball simply doesn’t exist!. How do you handball behind your back? Ahh.. go f*ck yourselves.”

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();