Powered by Blogger.

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatano hii, Dybala, Lukaku, Bale, Rice, Maguire, na wengine sokoni


Manchester United wanajiandaa kufanya mkataba wenye thamani ya pauni £120m na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala mwenye umri wa miaka 25, ikiwa mshambuliaji wao raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 25, ataondoka Old Trafford katika msimu wa kiangazi. (Sun)


Manchester City inaweza kupokea kitita cha pauni £15m ikiwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho atanunuliwa pauni £100m msimu huu. Manchester United wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 . (Sun)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anafahamu fika kuwa anaweza kukabiliana na mapambano ya kuendelea kubakia na Harry Maguire msimu wa kiangazi
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Clive Allen ansema kuwa klabu hiyo ya Kaskazini mwa Londonanaweza kutoa ”tangazo kubwa” kwa kusaini mkataba na mshambuliaji wa kiungo cha kati kutoka Wales Gareth Bale, ambayer sasa ana umri wa miaka 29, kutoka Real Madrid. (Talksport)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa West Ham, Declan Rice, mwenye umri wa miaka 20, anatarajiwa kukamilisha kikosi cha England kwa ajili ya kombe la washindi la Ulaya baada ya FA kukamilisha mkataba wa kumuhamisha kutoka jamuhuri ya Ireland. (Telegraph)
Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anafahamu fika kuwa anaweza kukabiliana na mapambano ya kuendelea kubakia na Harry Maguire msimu wa kiangazi, huku Manchester United ikiwa inamtaka mlinzi wa England mwenye umri wa miaka 26. (Leicester Mercury)

AC Milan wanamtaka Gianluigi Donnarumma aendelee kulilinda lango lao hadi walau 2024
Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Chelsea na Manchester United Peter Kenyon amezindua mpango wa ununuzi wa timu ya Bolton Wanderers. (sun)
Mlinzi wa Cardiff City Sol Bamba, mwenye umri wa miaka 34, ameiunga mkono upande wa Wales ili kuepuka kuondolewa kwenye Premier League. (Mirror)
Mazungumzo ya mkataba yameanza baina ya AC Milan na mlinada lango wao Gianluigi Donnarumma mwemye umri wa miaka 20 . Milan wako makini kurefusha mkataba na Mtaliano hadi walau mwaka 2024. (SportMediaset, via Calciomercato)
Schalke inatarajia kuishawishi Liverpool imuuze mshambuliaji wake Taiwo Awoniyi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21- raia wa nigeria kwa sasa anacheza kwa deni katika klabu ya ubelgiji ya Mouscron. (Liverpool Echo)
Hull City wanakusanya taarifa kumuhusu mlindalango wa Reading mwenye umri wa miaka 21 Luke Southwood, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni katika Eastleigh na ameichea timu ya vijana ya England , kabla ya msimu wa kuhama wa kiangazi. (Daily Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati cha Ajax Frenkie de Jong akiri kupewa kibarua cha kuiondoa real madrid kwenye Ligi ya championi
Mchezaji wa kiungo cha kati Ajax Frenkie de Jong, mwenye umri wa miaka 21, anasema Barcelona ilimuambia aiondoe nje ya Championi Ligi Real Madrid. Mjerumani huyo atajiunga na washindi wa La Liga katika msimu wa majira ya joto. (De Telegraaf, via Evening Standard)
Andres Iniesta anaamini kuwa mchezaji mwenzake wa kiungo cha kati Muhispania Sergi Samper, mwenye umri wa miaka 24, ataondoka Barcelona kujiunga na timu ya Jqapan ya Vissel Kobe. (Reuters)
Mashabiki wa Real Madrid wanapewa nafasi ya kupiga kurajuu ya ikiwa kila mchezaji wa timu hiyo anapaswa kuuzwa na ni nani anapaswa kuwa meneja ajaye wa klabu hiyo.(Marca – in Spanish)
North Ferriby United huenda wakawa na mmiliki mpya kabla ya kumalizika kwa msimu baada ya mmiliki wa sasa kubadili jina na kuiita East Hull. (Hull Daily Mail). AFC Wimbledon wanatarajia kuanza kujenga uwanja wao mpya katika Plough Lane mwezi Aprili au Mei. (Evening Standard)
Chanzo BBC.

No comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();